\”Chuo chetu cha Embu twaomba,
Ewe Mwenyezi ukibariki,
Tunapowahudumia wote wapate Elimu bora Mungu,
Tupe maarifa ili tufaulu.
Madhumuni ya taasisi yetu,
Nikuwapa wote mafunzo,
Ili Kesho waweze kujitegemea na kuwa vinara kote,
Tuwe kwenye kilele cha Kenya.
Tuwe Mwongozo wa Kenya yote,
Kielimu nidhamu na pia,
Nyanja zote tuwe mfano mwema ili majirani waige kwetu,
Tushikane, tusonge mbele.